Na RIPOTA
Jumapili, Januari 19, 2025
MRADI wa Imarisha Elimu unatazamiwa kuchangia mabadiliko makubwa kwenye masomo ya wanafunzi wa Shule za Upili za kutwa katika Kaunti Ndogo ya Thika. Mbunge wa Thika, Bi. Alice Ng’ang’a anasema amezidua mradi huo ili kuhakikisha wanafunzi wa eneo hilo wanahudhuria shule bila kuchelewa.
”Nimeanzisha mradi wa Imarisha Elimu ili kutoa fursa kwa wanafunzi wawe wakipata mankuli shuleni hasa uji na chakula cha mchana,” alieleieza mbunge huyo. Alidokeza kuwa atatumia mfuko wa fedha za ustawi wa maeneo mbunge (NG-CDF) kilipia wanafunzi hao Sh2,500 kwa muhula badala ya Sh18,000.
Kufuatia tangazo hilo wazazi wameshukuru juhudi zake na kusema kuwa ameelewa mzigo mzito waliokuwa wamebeba. Mbunge huyo alitaja baadhi ya Shule zitakaonufaika na mradi huo kama Kenyatta Girls Secondary, Jamhuri Secondary, Gatuanyaga, Magogoni, Garisson, Broadway,na Ngoliba. Halfa ya uzinduzi wa mradi huo ilifanyika Ijumaa, Januari 17, 2024 kwenye Shule ya Kenyatta Girls Secondary, Makongeni Thika.
Akizungumza kwenye hafla hiyo mbunge huyo aliwataka wazazi ambao watoto wao wana ujuzi wa kiufundi kama kuunganisha bomba za maji, umeme pia wanaoweza kuendesha bodaboda wafike katika afisi yake ili watafutiwe ajira. ” Iwapo mtoto wako ana Pasipoti pia ujuzi wa kiufundi mwambie awasilishe vyeti vyake afisini mwangu ili niweze kutafuta mbinu ya kuwasafirisha nchi za nje,” alisema.
Anashikilia kwamba kwa muda wa miaka mitatu iliyosalia anapania kuwahudumia wananchi wa eneo hilo ipasavyo. ”Nataka wapinzani wangu wanipe nafasi nifanyie wananchi kazi badala ya kushinda wakinipiga kisha ifikapo mwaka 2027 wataamua wenyewe,” akasema.
Mkurungezi wa elimu katika Kaunti Ndogo ya Thika Magharibi, Maurice Sifuna alishukuru juhudi za mbunge huyo zinazolenga kupunguzia wazazi mzigo wa karo. ”Ni mradi mzuri utakaotoa nafasi nzuri kwa wazazi kujikwamua kutokana mzigo wa karo,” alisema. Naye mwalimu mkuu wa Shule ya Kenyatta Girls Secondary Bi Mary Njoroge alisema wazazi watapata afueni kutokana na mradi huo. Wazazi wanapitia wakati mgumu kimaisha pia karo ya juu na mahitaji mengine kugharamia masomo ya wanao.
Post Views: 54