Connect with us

Hi, what are you looking for?

News

Shule ya MP Shah Chania High Yatamba Masomoni

Na RIPOTA WETU
Jumamosi, Januari 11, 2025
SHULE ya Upili ya MP Shah Chania High ya Thika, Kaunti ya Kiambu, ilifanikiwa kupata wanafunzi 22 waliozoa alama za A na A – kwenye mtihani wa kitaifa wa KCSE mwaka 2024.  Ijumaa, Januari 10, 2025 mwalimu mkuu wa Shule hiyo, James Gitau alijumuika na walimu wenzake pia wanafunzi shuleni humo kusherekea ufanisi wao. 
Kwenye matokeo hayo, wanafunzi wanne walifanikiwa kuandikisha alama ya A huku Shule hiyo ikizoa mini gredi ya alama 7.3591. Nao wanafunzi waliopata alama ya A – walikuwa 18.  ”Kusema ukweli tumepata matokeo ya kufurahisha kwani walimu walijikakamua kufunza wanafunzi wetu ambapo kama Shule tunajivunia ufanisi huo,” alisema. Jumla ya wanafunzi 337 wa shule ya Mp Chania walifanya mtihani huo na wengi walifanikiwa kupata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu.
Wanafunzi waliopata alama ya A ni Terrence Micah Musee, Wanjiku Lance Gathu, Nyambura Graig mwaniki na Wamaitha Prestons Ng’ang’a. Wazazi wengi waliohudhuria hafla hiyo walionekana kuwa wachangamfu huku wakimpongeza mwalimu mkuu kwa kuhakikisha wanafunzi wao wanadumisha nidhamu iliyochangia ufanisi huo.
Mwalimu Mkuu akizungumza na Jichonews dijitali alisema aliwashauri walimu wake kutumia taaluma yao kufunza wanafunzi wao na kusaidiana nao kwa mawaidha ili wawaze kutia fora masomoni. Aidha ameshukuru wazazi kwa kuitikia mwito wa upanzi wa mabweni shuleni humo jambo lililopunguza msongamano.
“Mwaka huu wa 2025 tutaweka mikakati kamili kuona kwamba tunapiga hatua zaidi,” alisema kinara huyo na kuongeza kuwa mipango walioweka kuhakikisha wanafunzi wanadumisha nidhamu wataendelea kuitilia maanani ili kufanikisha malengo yao. Alidokeza kuwa siri kuu ya ufanisi huo ilikuwa kumuweka Mungu mbele maana kila siku lazima wanafunzi wazingatie kufanya sala kabla ya kuanza masomo yao. Kadhalika alifafanua kuwa wanafunzi hao walikuwa watiifu na waliheshimu walimu wao sana. Pia alifunguka kuwa walikuwa wakikamilisha majaribio yao kwa wakati ambapo kufuatia mpangilio huo kila kitu kiliendeshwa vizuri.
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You May Also Like

News

Na RIPOTA WETU Jumamosi, Januari 11, 2025 SHULE ya Upili ya Thika High inajivunia wanafunzi wapatao 25 kuandikisha alama za A na A- kwenye...

Sports

Na RIPOTA WETU Jumanne, Januari 21, 2025 TIMU ya wanaume ya Simlaw na Jacaranda kila moja ilionyesha voliboli ya kuvutia na kunasa tikiti ya...

Sports

By Our Reporter Monday, September 8, 2025  THE National Commercial Bank of Africa (NCBA) men’s football team defeated Consolidated Bank 2-0 in 39th edition...

Sports

Na RIPOTA WETU Jumanne, Januari 21, 2025   SITA Mbili FC imerarua Young Shine FC kwa mabao 3-0 kwenye mechi  ya Kundi A Ligi...