Connect with us

Hi, what are you looking for?

Sports

Sita Mbili FC Yang’ata Huku KYSA/Cuk Ikiteleza Michuano Ya NWRL

Na RIPOTA WETU
Jumanne, Januari 21, 2025
 
SITA Mbili FC imerarua Young Shine FC kwa mabao 3-0 kwenye mechi  ya Kundi A Ligi ya Kanda ya Nairobi Magharibi (NWRL) iliyochezwa Jumapili, Januari 19, 2025 ugani Toi Primary, Nairobi. Nayo KYSA/Cuk ilitoka nguvu sawa bao 1-1 na Rongai Sports huku Kiserian Wenyeji ikivuna magoli 5-2 dhidi ya Maroon Young Stars. 
Young Shine imepata kichapo hicho ikiwa ni wiki moja baada ya kudhalilisha South B All Stars kwa mabao 6-0. KYSA/Cuk ilishindwa ujanja na wapinzani wao licha ya Reagy Odhiambo kutangulia kufunga. ”Mpira hudunda wala hatuna lingine tulikubali yaishe lakini lazima turudi mezani kupiga hesabu tena,” alisema Benson Godia kocha wa KYSA/CUK. Aliongeza kuwa itabidi wajitume kwa udi na uvumba wahakikishe wanavuna ushindi kwenye mechi ijayo ili vijana wapate motisha.
Sita Mbili FC ilishuka dimbani tayari kupiga shughuli za uhakika na kubeba alama tatu muhimu. Kikosi hicho chini ya kocha, Ken Aidha kilinyamazisha wapinzani wao pale Ray Amara alipopiga ‘hat trick.’ ”Vijana wangu wanajifunza soka kwenye kila mechi ingawa wapinzani wetu wana tupigia hesabu tofauti maana tulijiunga na kipute hicho baada ya kuibuka mabingwa wa ligi ya Kaunti,” anasema kocha huyo. Hata hivyo aliongeza kwamba wanafahamu kampeni za msimu huu sio mteremko lazima wajitume pia wamakinike.
Kwenye matokeo hayo, kocha George ‘Mandevu’ Omondi aliongoza Kiserain Wenyeji  FC kubeba ushindi wa pili. Ufanisi huo ulipatikana kupitia Philip Jagongo na Victor Ketikai waliopiga kombora mbili kila mmoja huku Peter Wanyama akitupia kimiani bao moja.  Maafande wa Maroon Young Stars wa kocha, Ali Sifuna walipata mabao ya kufutia machozi kupitia juhudi zake Omari Mandi na Hillary Katana waliotikisa wavu mara moja kila mmoja. ”Ninashukuru wachezaji wangu kusajili alama tatu muhimu maana wamepania makubwa kwenye kipute cha msimu huu,” alisema kocha wa Kiserian.
Naye Job Ochieng alifungia Karen Hospital FC bao la kufutia machozi ilipokubali kulala kwa mabao 3-1 mbele ya Jamhuri SA. Kwenye mfululizo wa matokeo hayo, Black Berets ilitandika Generation Sharpfoot FC  kwa mabao 2-1, RVSA iliadhibu 111-States kwa mabao 3-1, South B All Stars ilizaba All Blacks FC kwa mabao 2-0 huku Diguna FC ikiagana sare tasa na Laiser Hill Scorpions.
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You May Also Like

News

Na RIPOTA WETU Jumamosi, Januari 11, 2025 SHULE ya Upili ya MP Shah Chania High ya Thika, Kaunti ya Kiambu, ilifanikiwa kupata wanafunzi 22...

News

Na RIPOTA WETU Jumamosi, Januari 11, 2025 SHULE ya Upili ya Thika High inajivunia wanafunzi wapatao 25 kuandikisha alama za A na A- kwenye...

Sports

Na RIPOTA WETU Jumanne, Januari 21, 2025 TIMU ya wanaume ya Simlaw na Jacaranda kila moja ilionyesha voliboli ya kuvutia na kunasa tikiti ya...

Sports

By Our Reporter Monday, September 8, 2025  THE National Commercial Bank of Africa (NCBA) men’s football team defeated Consolidated Bank 2-0 in 39th edition...